IOM yasaidia wahamiaji waliokwama Libya

27 Februari 2015

Raia wa Senegal wamerejeshwa nchini kwao baada ya kukwama nchini Libya kutokana na mapigano.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limeandaa usafiri kwa wanaume hawa 133 kutoka mji wa Misrata kuelekea mjini Dakar kupitia Tunisia kwa njia ya basi na ndege.

Operesheni hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano na wizara ya mambo ya ndani ya Libya na mashirika ya misaada ya kibinadamu,

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Geneva, msemaji wa IOM Joel Millman amesema ni hatua ya kwanza kwenye mpango wa IOM wa kuwarejeshwa maelfu ya wahamiaji kutoka Libya na Misri. Tayari IOM imeshafanikiwa kuwarejesha kwao karibu wahamiaji 200,000 tangu mwanzo wa mzozo mwaka 2011. Licha ya mapigano yanayohatarisha safari hizo, IOM imesema changamoto kubwa ni kwamba wahamiaji hawa wengi hawana vitambulisho .

Kwa mujibu wa IOM, bado zaidi ya wamisri milioni moja na raia 300,000 kutoka Africa na Asia wanaishi Libya na wengi wao wangependa kurudi kwao, huku wakihitaji msaada wa kibinadamu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter