Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yarejesha makwao mamia ya raia wa Ethiopia kutoka Tanzania na Yemen

IOM yarejesha makwao mamia ya raia wa Ethiopia kutoka Tanzania na Yemen

Shirika la kimtaifa la uhamiaji IOM nchini Ethiopia  , Tanzania na Yemen juma hili limewasaidi Waethiopia 125 wengi wao wakiwa ni watoto wasio na wazazai  kurejea makwao kutoka Tanzania  na Yemen.

Kwa mujibu wa IOM, kati ya hao , 54 walirudishwa kutoka  Tanzania,  ikiwa ni pamoja na watoto sita ambao waliwekwa kizuizini na mamlaka zaidi ya nchi hiyo wakijaribu kufika Afrika Kusini na hivyo kukaa kizuizini kwa miezi minne kabla ya IOM kuratibu zoezi la kuwarudisha makwao.

Wengine 71 kutoka Yemen ambae ni watoto waliokuwa pekee yao ambao IOM inasema walivuka bahari ya Sham wakijaribu kuingia falme za Uarabuni hivyo kusalia katika sintofahamu. Watoto hao waliwekwa kizuizini nchini Yemen kwa takribani majuma  matatu kabla ya kunusuriwa na kurejeshwa makwao.

Mwaka jana shirika la kimataifa la uhamiaji IOM liliwasadia wahamiaji  raia wa Ethiopia zaidi ya 800 kurejea makwao kutoka Yemen ambapo kati yao 344 walikuwa watoto wasiokuwa na mlezi au wasindikizaji.