Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufilipino ni lazima utoe kipaumbele katika chakula na usalama wa lishe:UM

Ufilipino ni lazima utoe kipaumbele katika chakula na usalama wa lishe:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki ya chakula Hilal Elver amesema upatikanaji wa chakula chenye lishe ya kutosha bado ni changamoto nchini Ufilipino licha ya hatua zilizopigwa .

Bi Elver ameonya hayo leo akihitimisha ziara yake ya kwanza nchini humo na kuitaka serikali ya Ufilipino kuanzisha sera madhubuti ambayo inachagiza haki  ya chakula bora.

Ameongeza kuwa wakati uchumi wa taifa hilo umeanza kuonyesha nuru katika miaka ya karibuni fursa ya watu kupata chakula bora na lishe inayostahili inaendelea kuwa tatizo karibu katika nchi nzima hasa katika lishe duni akisistiza kwamba utapia mlo kwa watoto ni suala ambalo linatia hofu wakati zaidi ya watoto milioni 4 nchini humo wakiwa na matatizo ya kudumaa.