Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaanza tena kutoa 100% ya msaada wa chakula Uganda

WFP yaanza tena kutoa 100% ya msaada wa chakula Uganda

Shirika la Mpango wa Chakula Dudiani (WFP) nchini Uganda limeanza tena kutoa chakula kwa wakimbizi nchini humo kikamilifu baada ya kupigwa jeki ya Dola Milioni 17.7 za Kimarekani.Msaada huo unatarajiwa kuziba pengo la mahitaji ya chakula ya kuanzia mwezi April hadi mwezi Julai mwaka huu. Kutoka Uganda, John Kibego na maelezo kamili.

 (Taarifa ya John Kibego)

Mwakilishi wa WFP humo nchini Alice Martin-Daihirou gamesema, wamepokea Dola za Kimarekani milioni 15.4 kutoka serikali ya Marekani na nyingine milioni 2.3 kutoka serikali ya Australia.

Amefafanua kuwa fedha hizo zitasaidia kushughulikia mahitaji ya chakula kwa wakimbizi wapatao 303,000 na wananchi 157,000 walioathiriwa na njaa katika eneo la Karamoja.

Kutokana na pengo la ufadhili, shirika hilo la Mpango wa Chakula Duniani lililazimika kukata mgao wa chakula kwa 50% mwezi uliyopita.

Waliokimbia mapigano yalioibuka mwezi Disemba 2013 nchini Sudan Kusini na wakimbizi wenye mahitaji ya kipekee ndio hawakuathiriwa na mkato huo.