Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM Somalia akaribisha kuachiliwa kwa mateka:

Mwakilishi wa UM Somalia akaribisha kuachiliwa kwa mateka:

Mwakilishi wa Umoja wa mataifa nchini Somalia bwana Nicholas Kay, amekaribisha kuachiliwa kwa wafanyakazi wanne wa meli ya FV Prantalay 12 hapo februari 25 . Mateka hao walikuwa wakishikiliwa na maharamia wa Kisomali tangu April 18 mwaka 2010.

Bwana Kay amesema huko ni kushikiliwa kwa muda mrefu zaidi kuwahi kufanywa kwa mateka wowote waliotekwa na maharamia wa Kisomali. Watu hao ambao wote ni raia wa Thailand waliachiliwa na maharamia wa Kisomali na kukabidhikwa kwa uongozi wa jimbo la Galmudug.

Ameongeza kuwa ameshukuru kuona mateka hao wa muda mrefu hatimaye wameachiliwa kutoka Somalia na amewashukuru wote waliofanikisha hatua hiyo hususan uongozi wa Galmadug.

Mkakati wa kuachiliwa kwa mateka hao uliendeshwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uhalifu na vita dhidi ya madawa ya kulevya UNODC kwa ufadhili wa mfuko maalumu wa kukabiliana na uharamia pwani ya Somalia.