Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usaidizi wahitajika kwa wakimbizi wa Syria na wenyeji ili kudumisha amani Lebanon.

Usaidizi wahitajika kwa wakimbizi wa Syria na wenyeji ili kudumisha amani Lebanon.

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Lebanon, Sigrid Kaag amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuisaidia Lebanon wakati ambapo inakabiliana na matokeo ya mzozo wa Syria.

Amesema haya akitembelea maeneo ya Bekaa, wanapoishi zaidi ya wakimbizi 400,000 kutoka Syria. Amesisitiza umuhimu wa misaada ya kibinadamu na kimaendeleo kwa wakimbizi wenyewe lakini pia kwa wenyeji ili kuimarisha utulivu wa nchi.

Mtalaam huyu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kwamba Lebanon inahitaji usalama, na ulinzi wa haki za binadamu ili kuwa na utulivu wa kudumu.

Katika zaiara yake Bi Kaag amekutana na viongozi wa eneo la Bekaa, na amezungumza pia na wakimbizi wa Syria. Aidha ametembelea kiwanda cha kuzalisha nishati ya jua kilichofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP.