Ushirikiano wa Baraza Kuu na ECOSOC ni muhimu zaidi sasa: Kutesa

26 Februari 2015

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa amesema ushirikiano kati ya baraza hilo na lile la masuala ya uchumi na kijamii la umoja huo, ECOSOC ni muhimu zaidi hivi sasa ili kufanikisha ajenda za chombo hicho kinachotimiza miaka 70 mwaka huu tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza kwenye kikao cha kupitia ripoti ya utendaji ya mwaka 2014 ECOSOC, Bwana Kutesa amesema maudhui ya vikao vya kipindi hicho yalibeba ujumbe mzito wa kushughulikia changamoto zinazobuka ili kufikia malengo ya maendeleo ya milenia na kutumia kiuendelevu manufaa yanayopatikana.

Amesema matokeo ya vikao hivyo yatakuwa na mchango mkubwa wakati huu Umoja wa Mataifa unavyosongesha mashauriano ya kuandaa ajenda mpya ya maendeleo. Hata hivyo amesema

(Sauti ya Kutesa)

 “Katika kusonga mbele tunahitaji msisitizo zaidi kwenye dhima ya jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa katika kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa ajenda ya maendeleo baada ya mawka 2015. Na ikiwezekana matokeo ya mkutano wa tatu kuhusu ufadhili na maendeleo. Hii itahitaji uratibu zaidi na ushirikiano kati ya Baraza Kuu la ECOSOC.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud