Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatupaswi kushindwa na kuisahau Gaza: Mashirika ya Misaada.

Hatupaswi kushindwa na kuisahau Gaza: Mashirika ya Misaada.

Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa na yale ya kimataifa yasiyo ya kiserikali NGO’s yamesema yanatiwa wasiwasi na maendeleo madogo ya kujenga upya maisha ya watu walioathirika na vita Gaza na kutafuta mzizi wa mgogoro huo. Taarifa ya Flora Nducha inafafanua..

(TAARIFA YA FLORA )

Ikiwa ni miezi sita imepita tangu muafaka wa kusitisha mapigano Gaza hapo Agosti 26 mwaka jana na kumaliza vita vilivyodumu kwa wiki saba baina ya majeshi ya Israel na makundi ya Kipalestina yenye silaha kwenye ukanda wa Gaza , bado vikwazo vya Israel dhidi ya Gaza vinaendelea huku mchakato wa kisiasa na uchumi ukizidi kudidimia na hali ya maisha ya watu kuwa mabaya zaidi.

Mashirika hayo ya misaada yanataka Gaza isisahaulike hasa kwa misaada muhimu ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watu .

Kwa kutambua umuhimu huo serikali ya Japan imetoa dola za Kimarekani milioni 32.2 kama mchango wake kwa Shirika la Umoja wa mataifa la msaada kwa  wakimbizi wa Kipalestina UNRWA.

Mchango huo utasaidia mahitaji ya UNRWA , ujenzi mpya wa Gaza, msaada wa dharura kwa wakimbizi wa Kipalestina walioathirika na vita vya Syria na mahitaji mengine ya UNRWA.