Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Picha ya watoto wa mitaani yashinda tuzo la WFP

Picha ya watoto wa mitaani yashinda tuzo la WFP

Shirika la Mpango wa chakula duniani WFP limeandaa mashindano ya picha kuhusu mlo wa familia, likisema kwamba kula chakula kwa pamoja ni utamaduni unaopatikana duniani kote ambao unatuunganisha licha ya tofauti za kimila.

Mpishi maarufu Jamie Oliver na raia wa kawaida wameshirikiana katika kuchagua picha bora. Miongoni mwa washindi watatu ni Darine Ndihokubwayo kutoka Burundi.

Picha yake inaonyesha watoto wa mitaani wanaochangia chakula kwenye sinia kubwa, kwa msaada wa shirika lililoanzishwa na Darine mwenyewe na vijana wenzake.

(Sauti ya Darine-1)

Darine ambaye ni mfanyakazi wa shirika la kimataifa nchini Sudan Kusini amesema kuwajali watoto hao na kuwapatia chakula kumewasaidia kwenye maisha yao..

(Sauti ya Darine-2)

WFP imesema lengo la kazi zake kote duniani ni kuhakikisha kwamba familia zinaweza kuendelea kupika na kula kwa pamoja kila siku, hata zikiwa kwenye mazingira magumu, na hivyo kubaki na matumaini.