Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalaani vikali utekwaji wa Wakristo wa Syria unaofanywa na ISIL:

Baraza la usalama lalaani vikali utekwaji wa Wakristo wa Syria unaofanywa na ISIL:

Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali kitendo cha ISIL kuwateka zaidi ya Waashuri 100 hapo Februari 23 mwaka huu huko Kaskazini Mashariki mwa Syria pamoja na uharibifu na unajisi wa Wakristo na maeneo mengine ya kidini.

Kwa mujibu wa baraza la usalama vindondo hivyo kwa mara nyingine vinadhihirisha ukatili wa ISIL kundi linalowajibika kwa uhalifu na ukatili dhidi ya maelfu ya watu kutoka Imani, makabila na mataifa mbalimbali bila kujali thamani ya utu.

Wajumbe hao wa baraza wamelaani vitendo vyote vya ghasia dhidi ya raia vikiwemo vinavyotekelezwa kwa misingi ya kikabila, kidini au Imani.

Baraza limetaka kuachiliwa mara moja na bila vikwazo vyoyote kwa wale wote waliotekwa na ISIL, Al-Nusra Front na watu wote binafsi, makundi na vyombo vinavyohusiana na Al-Qaida,na kusisitiza kwamba watu wanaohusika na vitendo hivyo lazima wawajibishwe.