Mataifa ya Afrika ya Mashariki yabadilisha mawazo ya vita dhidi ya umasikini na kutokuwepo kwa usawa:
Wawakilishi kutoka Mataifa ya Afrika ya mashariki wanakutana Nairobi Kenya kwenye kongamano maalum ili kubadilishana uzoefu wa kukabiliana na umasikini na kutokuwepo kwa usawa .
Kongamano hilo la mawaziri wa maendeleo ya jamii limeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ni la kwanza la aina hiyo.
Nchi 15 kutoka ukanda wa Afrika ya Mashariki wanashiriki kata kongamano hilo. Mada maalumu ya kongamano hilo ni “Haki ya kimataifa” ikijikita katika kushirikiana uzoefu na sera katika masuala kama kupunguza umasikini na kutokuwepo kwa usawa.
Mjadala huo utachangia katika maendeleo ya ajenda ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa baada ya mwaka 2015. Masuala mengine muhimu wanayojadili ni ajira kwa vijana na maendelo ya ujuzi, ukuaji wa idadi ya watu na inavyochangia katika maendeleo ya kijamii.
Mwisho wa kongamano hilo kunatarajiwa mapendekezo na kupitishwa kwa azimio la mawaziri hapo kesho Februari 26.