Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afghanistan imepiga hatua mapambano dhidi ya uteswaji: UNAMA

Afghanistan imepiga hatua mapambano dhidi ya uteswaji: UNAMA

Ripoti ya Umoja wa Maraifa iliyotolewa leo kuhusu utesaji na uwekwaji vizuizini kutokana na migogoro nchini Afghanistan, inaonyesha kuwa hatua zimepigwa na hivyo kukaribisha ahadi mpya za kuongeza juhudi ili hatimaye kukomesha utesaji.

Kwa mujibu wa mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan na mkuu wa ujumbe wa umoja huo nchini Afghanistan UNAMA,  Nicholas Haysom juhudi za serikali ya nchi hiyo ziko dhahiri katika miaka miwili ilitopita.

Hata hivyo amesema mengi yanapaswa kufanyika na kukaribisha mpango mpya wa utekelezaji mpango mpya wa kukomesha uteswaji.

Serikali ya Afghanistan pamoja na mambo mengine  inakusudia kufanya mageuzi ya kisheria kupitisha mkataba dhidi ya utesaji, na kuendesha mafunzo kuhusu suala hilo kama sehemu ya mpango mpya wa kukomesha uteswaji.