Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yataka juhudi zaidi kukomesha surua Ulaya

WHO yataka juhudi zaidi kukomesha surua Ulaya

Ofisi ya shirika la afya ulimwenguni WHO kanda ya Ulaya linawataka watunga sera, wafanyakaazi katika sekta ya afya na wazazi hima kuhakikisha utolewaji wa chanjo dhidi ya surua ili kukomesha mlipuko unaotokea katika nchi za bara hilo sasa na siku za usoni.

Tangazo hili la WHO linakuja wakati huu ambapo visa kadhaa vya surua vinatajwa . Mathalani  mwaka 2014 pekee WHO inasema kulikuwa na zaidi ya visa 22,000 vya surua na hivyo kutishia lengo la ukanda huo la kukomesha ugonjwa huo ifikapo mwaka 2015.

Taarifa ya shirika hilo la afya ulimwenguni inamnukuu Mkurugenzi wa WHO kanda ya Ulaya Dr Zsuzsanna Jakab akisema licha ya mafanikio ya kupunguza surua kwa asilimia 96 barani humo, juhudi zaidi zinahitajika bila kuchelewa ili kupunguza pengo la kinga.

Amesema kuwa haikubaliki ya kwamba licha  ya juhudi za miaka 50 katika kuhakikisha chanjo salama na yenye ufanisi, surua inaendelea kugharimu maisha , fedha na muda

Surua aina ya D8 ndiyo inayotamalaki zaidi barani Ulaya