Vikwazo dhidi ya Yemen vyaimarishwa

24 Februari 2015

Baraza la Usalama leo kwa kauli moja limepitisha azimio la kuongeza muda wa vikwazo dhidi ya Yemen.

Vikwazo hivyo vimeongezewa muda hadi Februari 2016 na vinalenga kuzuia biashara na usafiri wa watu wanaodaiwa kushirikiana na kundi la ugaidi la Al-Qaida.

Wanachama wa Baraza hilo wameeleza wasiwasi wao kuhusu hali ya usalama na uchumi nchini humo ambayo inaendelea kuzorota, wakikariri kwamba ghasia siyo suluhu kwa tatizo la kisiasa.

Baraza la usalama limeiomba jamii ya kimataifa iendelee kusaidia Yemen katika wakati huo wa mpito.

Limetaka pia kuongezwa kwa mamlaka ya ofisi ya Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo ili aweze kuisaidia serikali kuunda katiba mpya, kuandaa uchaguzi na kutekeleza mabadiliko katika sekta ya usalama.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter