Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yataka kuachiliwa mara moja watoto waliotekwa Malakal:

UNICEF yataka kuachiliwa mara moja watoto waliotekwa Malakal:

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema linahofia usalama wa wavulana 89 na waalimu sita waliotekwa juma lililopita kwenye eneo la Wau Shilluk jimbo la upper Nile Sudan Kusini. Flora Nducha na taarifa kamili.

(Taarifa ya Flora Nducha)

Wavulana hao baadhi wakiwa naumri wa miaka 13 wametekwa nakundi la watu wenye silaha wasiojulikana. Na mpaka sasa hawajapatikana.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa Sudan Kusini afisa mawasiliano wa UNICEF mjini Juba John Budd amesema UNICEF inatoa wito wa kuachiwa mara moja wavulana hao na hatua zinachukuliwa kuhakikisha wanaachiliwa

(CLIP YA John Bud)

"Tumejulishwa kuwa wametekwa ili watumikishwe jeshini na tunalaani vikali kitendo hicho na tunatoa wito kwamba watoto hawa warudishwe haraka iwezekanavyo shuleni ili waendelee na mitihani na masomo yao. Tunafanya bidii ili waachiwe huru, na tuna wasiwasi mkubwa kwamba kama makundi ya waasi yataanza kulenga shule, basi wazazi hawatapeleka wavulana shuleni."