Twahitaji rasilimali zaidi kutokomeza Ebola: Dk. Nabarro

20 Februari 2015

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola Dkt. David Nabarro amesema suala la kutokomeza kabisa Ebola ni jukumu zito linalopaswa kufanyika kwa kushirikisha kwa kina nchi zilizoathirika zaidi na ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani, Bwana Nabarro amefananisha jukumu hilo na kutafuta sindano kwenye nyasi kavu akisema inapaswa kusaka wagonjwa popote pale walipo na kufuatilia wale waliokuwa karibu nao.

Amesema hilo linawezekana kwa ushirikiano na k wamba..

(Sauti ya Dkt. Nabarro)

“Kwa kuwa kuna mengi ya kufanya ili kutokomeza kabisa ugonwja na wakati  huo huo kuanza kipindi cha mpito cha kurejesha huduma za msingi na kujikwamua, Umoja wa Mataifa unahitaji kuendelea kufanya kazi kwa karibu zaidi na nchi zilizoathirika na jamii zao.”

Naye Mkurugenzi msaidizi wa shirika la Afya duniani, WHO anayehusika na dharura za magonjwa Dkt. Bruce Aylward amesema mkakati wa kutokomeza kabisa Ebola upo halikadhalika miundombinu lakini..

(Sauti ya Dkt. Aylward)

“Hatuna fedha za kutosha kufanikisha kututoa hapa tulipo na kukumaliza kabisa ugonjwa. Pia kuna hatari kubwa kwamba watu wataacha kuangalia janga hilo na kujikita katika mahitaji yanayotakiwa ili kumaliza ugonjwa  huu.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud