Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wataka uwezo dhidi ya majanga uimarishwe

Viongozi wataka uwezo dhidi ya majanga uimarishwe

Viongozi mbalimbali,  watunga sera na wataalam wamesema kujenga uwezo dhidi ya majanga  ni moja ya changamoto kubwa ya maendeleo inayokabili ukanda wa Asia na Pasific ambao ujko katika hatari kubwa ya kukumbwa na majanga

Wakihudhuria mkutano wa ukanda huo kuhusu kupunguza majanga, maendeleo na uwezeshaji wa kifedha uliondaliwa na tume  ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na kijamii kwa ajili ya Asia na Pasific (ESCAP),  wamesema licha ya ukuaji wa kasi wa uchumi nchi nyingi zinazoendelea hususani zilizo na uchumi mdogo zinakabiliwa na hatari ya majanga.

Viongozi hao wamependekeza uandaaji wa sera katika sekta mbalimbali na utekelezaji katika kukabiliana na majanga kwa kupanua wigo.

Mkutano huu unafanyika mwezi mmoja kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kupunguza majanga utakaofanyika Sendai nchini  Japan.