Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atoa wito tarehe ya uchaguzi isibadilishwe Nigeria

Ban atoa wito tarehe ya uchaguzi isibadilishwe Nigeria

Kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu nchini Nigeria hadi Machi 28 na Aprili 11, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa wito kwa serikali ya Nigeria na Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo, INEC, zihakikishe kuwa tarehe hizo mpya hazibadilishwi, kulingana na katiba ya Nigeria.Amekaribisha ahadi ya wagombea urais kuheshimu ratiba mpya ya uchaguzi.

Katibu Mkuu amesifu hatua zilizopigwa na INEC katika maandalizi ya uchaguzi, zikiwemo kutoa vyeti vya kudumu vya kupigia kura.

Ametoa wito kwa taasisi zote husika ziendelee kushirikiana na INEC ili kuhakikisha kuwa wapiga kura wote wanaweza kufurahia haki yao kikatiba ya kushiriki katika uchaguzi kwa uhuru na bila kutishwa.

Aidha, Ban ameelezea kusikitishwa mno na ripoti za machafuko yanayohusiana na uchaguzi huo. Ametoa wito kwa viongozi wote wa kisiasa kutimiza ahadi zao chini ya makubaliano ya Abuja, na kujiepusha na kauli chochezi, pamoja na kulaani mara moja kauli zozote kutoka kwa wafuasi wao ambazo zinaweza kuchochea ghasia au kuvuruga harakati za uchaguzi.

Stephanie Dujjaric ni msemaji wa  Umoja wa Mataifa

(SAUTI DUJJARIC)

“Katibu Mkuu amewasisitiza Wanigeria kuwa  Umoja wa Mataifa utakuw auanfuatili amaendelo nchini humo na anatoa uungwaji mkono mkamilifu katika wakati huu muhimu. Mwakilshi wake nchini humo Mumahed Ibn Chambas ataendelea kujihusiah na mamalaka za Nigeria katika majuma yajayo.”