Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udhibiti wa bahari waangaziwa kimataifa

Udhibiti wa bahari waangaziwa kimataifa

Jinsi ya kudhibiti maeneo ya bahari kuu ni mada ya kongamano linalofanyika mjini Roma, Italia likileta pamoja wataalamu mbali mbali ikiwemo wa Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO.

Dixon Waruinge kutoka Mkataba wa Nairobi kuhusu udhibiti wa bahari, kwenye Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira, UNEP, ameeleza athari zinazokumba bahari hizo.

(Sauti ya Dixon)

Lengo la mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano wa taasisi na mashirika ya kimataifa, ili kuongeza udhibiti wa uvuvi na utunzaji wa bayoanuai duniani kote.

Hata hivyo mtalaam wa UNEP amesema katika ukanda wa Afrika ya Mashariki ni muhimu kuboresha pia utunzaji wa bahari zilizo ndani ya mipaka ya nchi.

(Sauti ya Dixon-2)