Haki ya kijamii izingatiwe sambamba na utu: Ban

20 Februari 2015

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya haki za kijamii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amesema ni lazima jamii ya kimataifa ijitahidhi kujenga dunia ambayo watu wote wanaweza kuishi na kufanya kazi kwa uhuru, utu na usawa.Priscilla Lecomte na ripoti kamili.

(Taarifa ya Priscilla)

Katika ujumbe wake Ban amesisitiza wito wa kuhakikisha usalama wa kiutu na haki sawa pamoja na heshima kwa makundi yote ya kijamii.

Nalo shirika la kazi duniani ILO limesema utumikishwaji wa watu ukomeshwe likitaka viongozi kupambana na tabia hiyo. Hata hivyo mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki Alfred De Zayas analaumu utandawazi.

(Sauti ya De zayas)

"Utandawazi unapaswa na unatakiwa kusaidia haki ya kijamii lakini kwa kuwa unaendeshwa kwa misingi ya faida ndiyo maana hakuna makabiliano na ushirikianao katika majadiliano" 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter