Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada zaidi yamiminika kwa wakimbizi Sudan: OCHA

Misaada zaidi yamiminika kwa wakimbizi Sudan: OCHA

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kutahimini na kusaidia maelfu ya wakimbizi kufuatia mapigano kati ya vikosi vya serikali na vikundi vyenye silaha Kaskazini mwa Darfur nchini Sudan na baadhi ya maeneo ya Jebel MarraKwa mujibu wa chapisho la ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya kibinadamu OCHA, zaidi ya watu 7,000 wamepoteza makazi kufuatia machafuko na hivyo wanahitaji misaada ya dharura.OCHA inasema hadi kufikia Februari 12, shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesajili wakimbizi zaidi ya 7,000 wanaojihifahdi katika kituo cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa Darfur UNAMID  huko Um Baru.UNAMID kwa upande wake inatoa ulinzi wa usinidikizwaji katika kusaidia ufikishwaji wa misaada huku WFP ikikaririwa kutoa mgawo wa chakula cha mwezi mmoja kwa wakimbizi walioko Um Baru, maji, huduma za kujisafi na virutubisho.

Mashirika mengine yanayotoa misaada tofauti jimboni humo ni pamoja na lile la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  UNICEF, na asasi nyingine za kimataifa.