Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya digitali kulinda mapezi ya papa

Teknolojia ya digitali kulinda mapezi ya papa

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limebuni mbinu inayotumia teknolojia ya kidigitali, ISharkFin ili kufuatilia hatma ya papa walio kwenye orodha ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka.

Programu hiyo ya kiteknolojia inavishwa ndani  ya papa na kuwezesha kumtambua papa kupitia pezi lake.

Kwa mujibu wa Monica Barone mtalaam wa  FAO, wavuvi huwaua papa kwa wingi kwa ajili ya mapezi yao.

Nchini China, kimila, pezi la papa ni chakula chenye bei kubwa sana, kwa hiyo biashara kubwa ya mapezi imesababishwa na mila za nchi za Asia”

Akaendea mbali zaidi kuelezea jinsi teknolojia hiyo..

Mbinu hii ni muhimu sana ili kuboresha takwimu kuhusu papa duniani. Itasaidia sana maofisa wa forodha ambao hawajui kutofautisha papa kwa kuangalia mapezi yanayouzwa. Itasaidia kutekeleza utunzaji wa aina za papa wanaohifadhiwa sasa.”

Mwaka 2013, aina tano za papa zimeorodheshwa kwenye mkataba kuhusu biashara ya kimataifa ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka duniani.