Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya chakula na lishe Ufilipino kutathminiwa

Hali ya chakula na lishe Ufilipino kutathminiwa

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya chakula Hilal Elver, kuanzia Ijumaa atakuwa na ziara ya siku saba nchini Ufilipino kutathmini hali ya chakula na lishe.

Taarifa ya ofisi ya haki za binadamu imesema tathmini hiyo inazingatia ukweli kuwa licha ya maendeleo yaliyopatikana karibuni katika sekta hiyo, bado hali ya upatikanaji wa chakula cha kutosha na lishe bora ina mkwamo hususan baada ya kimbunga Haiyan.

Kwa mantiki hiyo Bi. Elver ataangalia jitihada zinazochukuliwa kuhakikisha kuna chakula na lishe ya kutosha na vikwazo vya kitaifa na kimataifa vya kufanikisha suala hilo.

Ziara ya Bi. Elver inafuatia mwaliko wa serikali ya Ufilipino na ni ya kwanza kufanywa na mtaalamu wa haki ya chakula.

Matokeo na mapendekezo ya ziara hiyo yatawasilishwa mbele ya Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi Machi mwakani.