UNIOGBIS yaongezewa mwaka mmoja zaidi

18 Februari 2015

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza kwa mwaka mmoja zaidi muda wa ujumbe wake nchini Guinea-Bissau, UNIOGBIS.

Uamuzi huo umo katika azimio lililopitwa leo na Baraza hilo ambapo kipindi kitaanzia tarehe Mosi mwezi ujao hadi tarehe 29 Februari mwakani.

Azimio hilo pamoja na kuongezaz muda wa ujumbe huo limepongeza kazi ya UNIOGBIS huku likiitaka ofisi hiyo ipatie vipaumbele mjadala shirikishi wa kisiasa nchini Guinea Bissau na maridhiano ya kitaifa.

Halikadhalika imeutaka ujumbe huo ipatie mamlaka za kitaifa na wadau husika ushauri wa kimkakati na kiufundi katika utekelezaji wa marekebisho ya sekta ya  usalama wa taifa na utawala wa sheria.

Azimio hilo pia limesititiza usaidizi wa mamlaka za kitaifa katika kuendeleza usimamizi wa haki za binadamu na ujumuisha wa masuala ya jinsia kwenye ujenzi wa amani kwa mujibu wa maazimio tangulizi ya baraza hilo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter