Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi dhidi ya raia yakomeshwe Syria: de Mistura

Mashambulizi dhidi ya raia yakomeshwe Syria: de Mistura

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Staffan de Mistura, ametaka kukomeshwa hima kwa makombora mazito na mashambulizi dhidi ya raia hususan mjini Allepo. Taarifa kamili na Asumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York muda mfupi baada ya kulihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa de Mistura amesema kuendelea kwa mapigano katika maeneo mbalimbali nchini Syria kunazidi kuzorotesha hali ya kibinadamu na kufuta matumaini ya kufikiwa kwa amani .

 (SAUTI DE MISTURA)

"Kwa kuzingatia kuwa ni jukumu letu kuwalinda raia wa Syria popote walipo huku tukiwa na matumaini yakupata suluhu la kisiasa . Ni kama ugonjwa, ukiwa huna tiba lakini angalau lazima usisitize upunguzwaji wa ukatili huu wa silaha nzito."

Amesisitiza pande kinzani nchini Syria kuruhusu ufikishwaji wa misaada ya kibinadamu na kusisitiza kuendelea kwa majadiliano ya suluhu ya mgogoro nchini humo.