Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio yasalia kuwa mkombozi wa wengi

Radio yasalia kuwa mkombozi wa wengi

Redio inasalia kuwa chombo muhimu kwa ustawi wa jamii na makundi mbalimbali barani Afrika ambapo wafanyabiashara, wanamuziki na wengineo hutegemea taarifa kupitia redio ili kuchukua uamuzi wenye tija katika kazi zao za kila siku za kujiongezea kipato. Mathalani huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, ambako Langi Stany wa Radio washirika Radio Umoja ameweza kuvinjari maeneo mbali mbali na kupata maoni ya watu kuhusu umuhimu wa radio wakati huu ambapo baadhi ya watu wanadai imepitwa na wakati.