Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano Ukraine yamevuruga mfumo wa huduma za afya- WHO

Mapigano Ukraine yamevuruga mfumo wa huduma za afya- WHO

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa vituo 78 vya afya vimeharibiwa katika mapigano nchini Ukraine kufikia sasa, zikiwemo hospitali 6 katika wiki mbili zilizopita.

WHO imesema kuwa mfumo wa kuwa kuwahudumia wagonjwa umevurugwa, na eneo la Donetsk linakumbwa na uhaba wa vifaa tiba, zikiwemo dawa za chanjo.

Kwa mujibu wa WHO, kumekuwa na ongezeko la visa vya ugonjwa wa kifua kikuu katika maeneo yasiyodhibitiwa na serikali, na ongezeko la maambukizi ya HIV kwa watoto kutoka kwa akina mama kwa sababu ya uhaba wa dawa.

WHO imesema imeweka vituo saba vya kuhamahama vya huduma za matibabu za dharura, na kwamba tani kumi za vifaa tiba zinapelekwa eneo la Donbas.