Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalaani mashambulizi yaliyofanywa na Boko Haram nchini Chad

Baraza la usalama lalaani mashambulizi yaliyofanywa na Boko Haram nchini Chad

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi dhidi ya Chad yaliyofanywa Ijumaa na kundi la kigaidi lenye makao yake nchini Nigeria, Boko Haram.

Katika shambulio hilo kwenye eneo liitwalo Ngouboua magaidi waliua raia pamoja na vongozi wa kimila na kujeruhi watu kadhaa. Mnamo Februari nane kundi hilo pia lilifanya mashambulizi huko Kerawa nchini Cameroon ikiwa ni siku mbili kabla ya mashambulizi nchini Niger katika eneo liitwalo Diffar.

Taarifa ya baraza la usalama imelaani kuendelea kwa mashambulizi yanayotekelezwa na Boko Haram.

Wajumbe wa baraza hilo wamesema aina yoyote ya ugaidi ikiwamo vitendo vya kundi hilo vinahatarisha usalama na amani na ya kimataifa.

Wamesisitiza kuwa vitendo vyote vya ugaidi ni uhalifu na havikubaliki bila kujali sababu zake. Pia wamesisitiza haja ya kuwafikisha  katika vyombo vya sheria watekekezaji  , wapangaji wa matukio hayo, wawezeshaji na wadhamini.

Baraza la usalama limetaka nchi wanachama kushirikiana na mamlaka husika ili kutekeleza hilo