Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambulizi mjini Copenhagen, Denmark

Ban alaani mashambulizi mjini Copenhagen, Denmark

Mashambulizi yaliyosababisha vifo vya watu wawili katika mji mkuu wa Denmark, Copenhagen yamelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari mtu mmoja alifyatua risasi kwenye kusanyiko la uhuru wa kujieleza Jumamosi huku mlipuko mwingine ukifanyika karibu na hekalu Jumapili.

Mtu mmoja ameripotiwa kuuwawa na askari watatu kujeruhiwa katika shambulio la Jumamosi katika magahawa . Katika shambulio la jumapili Myahudi mmoja aliuwawa na askari wawili kujeruhiwa katika sinagogi karibu na hekalu kuu mjini Copenhagen

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa imelaani vikali mashambulio mawili. Katibu Mkuu amenukuliwa akisema hakuna uhalali wa mashambulizi dhidi ya raia na kusisitiza umuhimu wa uhuru wa kuijeleza na kuvumiliana.

Amesema vita dhidi ya uyahudi, ubaguzi wa rangi au udini havina nafasi katika dunia ya leo. Bwana Ban ameelezea mshikamano wa Umoja wa Mataifa na watu na mamlaka za Denmark.