Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashauriano yaendelee wakimbizi Um Baru wapate makazi ya muda:UNAMID

Mashauriano yaendelee wakimbizi Um Baru wapate makazi ya muda:UNAMID

Naibu Mwakilishi wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, Abdul Kamara amefanya ziara eneo la Um Baru jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan ambako wakimbizi wapya wa ndani wamesaka hifadhi karibu na ofisi za ujumbe huo.

Maelfu ya raia wengi wao wanawake na watoto walikimbia makazi yao mwezi uliopita na kusaka hifadhi eneo hilo kufuatia mapigano kati ya vikosi vya serikali na vikundi vilivyojihami.

Baada ya mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale yasiyo ya kiraia kwenye eneo hilo Bwana Kamara amesisitiza umuhimu wa jitihada za pamoja ili kuwapatia wananchi hao huduma muhimu kama vile maji, afya, malazi na nyinginezo.

Amesema amevutiwa na kazi inayoendelea na kiwango cha uratibu alichoshuhudia katika kukabiliana na changamoto hiyo ya ukosefu wa huduma za kibinadamu.

Bwana Kamara amependekeza mashauriano zaidi ili kupatia suluhu hoja ya eneo la kuweka makazi ya muda kwa wakimbizi hao sambamba na kuboresha mazingira yao ya maisha.