Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana bado ni wachache kwenye radio: UNESCO

Vijana bado ni wachache kwenye radio: UNESCO

Wakati tukielekea siku ya Radio duniani Februari 13, shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limesema idadi ya vijana waandaji na watangazaji wa vipindi vya radio duniani bado ni ndogo.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema vijana wa kike na wa kiume ni wachache sana kwenye sekta ya Radio, halikadhalika vipindi vyenye ujumbe thabiti kwa kundi hilo.

(Sauti ya Bokova)

“Ubaguzi wa aina hii unachochea fikra potofu na kusababisha ukosefu wa usawa. Vijana wanachukua hatua wakiwa kama raia na waandishi wa habari wa kujitegemea na vyombo vingi vikubwa vya habari vinategemea kazi zao, lakini tunapaswa kuchukua hatua zaidi.”

Mkuu huyo wa UNESCO akatoa pendekezo.

(Sauti ya Bokova)

“Kwa kuwasaidia vijana kupitia elimu na mafunzo kwenye sekta ya vyombo vya habari kwenye maudhui, tunaweza kusaidia kujenga jamii shirikishi na yenye ustawi.”