Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nani atafadhili malengo endelevu, SDGs?:UNCTAD

Nani atafadhili malengo endelevu, SDGs?:UNCTAD

Wiki hii katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imekuwa na mkutano wa kujadili fursa ya biashara katika kufanikisha malengo endelevu ya maendeleo, SDG yatakayoanza kutekelezwa mwezi Septemba mwaka huu baada ya kufikia ukomo kwa malengo ya maendeleo ya Milenia MDGs yaliyopitishwa mwaka 2000. Mara baada ya mkutano huo, Assumpta Massoi wa Idhaa hii alipata fursa ya kumhoji Katibu Mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kituyi kuhusu mkutano huo na mustakhbali wa biashara kwa maendeleo ya nchi zinazojikwamua kama zile za Afrika. Kwanza anaanza kufafanua yale waliyokubaliana kwenye mkutano huo wa siku moja.