Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahanga wa janga la Lampedusa ni kubwa kuliko awali: UNHCR

Wahanga wa janga la Lampedusa ni kubwa kuliko awali: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeshtushwa na taarifa zinazodokeza kuwa idadi halisi ya watu ambao wanasakwa kufuatia la Lampedusa  lililoripotiwa Jumatatu ni 300 tofauti na iliyoripotiwa awali. Taarifa kamili na Grace Kaneiya

(Taarifa ya Grace)

Mkurugenzi wa UNHCR barani Ulaya Vincent Cochetel amesema kwa mujibu wa walinzi wa pwani ya Italia na manusura wa janga hilo, watu hao ni wahamiaji na wakimbizi kutoka nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara waliondoka Libya wakiwa kwenye  boti nne tofauti.

Taarifa za awali zilisema watu 29 walifariki dunia kwenye boti moja huku Zaidi ya manusura Zaidi ya 110 wakifanikiwa kutia nanga Lampedusa baada ya kuokolewa.

Manusura hao wameiambia UNHCR kuwa waliondoka Libya na wamekaa baharini kwa siku kadhaa bila chakula wala maji na kwamba zaidi ya watu 200 kutoka vyombo viwili bado hawajulikani waliko halikadhalika chombo kingine ambacho abiria wake mdogo zaidi ni mtoto mwenye umri wa miaka 12.

UNHCR imesisitiza hofu yake kuhusu ukosefu wa mbinu za kusaka manusura kwenye bahari ya Mediteranian ikisema operesheni Triton inayosimamiwa na mamlaka ya udhibiti mipaka ya Ulaya, hailengi kutafuta manusura na kuwaokoa.

Babar Baloch ni msemaji wa UNHCR

"UNHCR inatoa wito kwa Ulaya kuimarisha uwezo wake wa kutafuta na kuokoa watu kwa sababu watu hao ambao wako tayari kufanya lolote ili kupata hifadhi Ulaya, wataendelea kujaribu safari hiyo na maisha mengine yatapotezwa tusipokuwa na mfumo unaofanya kazi wa kutafuta na kuokoa watu."