Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujiamini ni mwarobaini kwa nchi maskini kuibuka kibiashara:UNCTAD

Kujiamini ni mwarobaini kwa nchi maskini kuibuka kibiashara:UNCTAD

Katibu Mkuu wa Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi amesema ukosefu wa kujiamini ndio kikwazo kwa nchi zinazoendelea kutumia biashara ili kuweza kujikwamua.Dkt. Kituyi amesema hayo mjini New York, alipohojiwa na Idhaa hii kando mwa mkutano wa UNCTAD wa kuangalia nafasi ya biashara katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDG.

(Sauti ya Dkt. Kituyi)

Huku akisema hitimisho la mazungumzo ya Doha yaliyokwama kwa miaka 13 sasa kuwa ndiyo suluhu ili biashara kuwa msingi wa maendeleo kwa nchi hizo, Dkt. Kituyi akaenda mbali zaidi.

(Sauti Dkt. Kituyi)

Mahojiano kamili na Mkuu huyo wa UNCTAD yanapatikana kwenye tovuti yetu.