Ban alaani kuuawa kwa mratibu wa UM nchini Guinea

Ban alaani kuuawa kwa mratibu wa UM nchini Guinea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani vikali mauaji ya Thierno Aliou Diaoune, Mratibu wa kitaifa wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa ujenzi wa amani nchini Guinea, ambayo yalifanyika katika mji mkuu, Conakry, mnamo Februari 6, 2015.

Taarifa ya msemaji wake imesema Bwana Diaoune alikuwa mdau wa kuaminika wa Umoja wa Mataifa na mtu aliyepigania ujenzi wa amani, demokrasia na haki za binadamu nchini Guinea bila kuchoka.

Katibu Mkuu amekaribisha tangazo la serikali la kufanya uchunguzi wa kina kahusu mauaji ya Bwana Diaoune, huku akituma salamu za rambi rambi kwa familia yake.