Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu dhidi ya Anwar Ibrahim ni pigo la demokrasia:IPU

Hukumu dhidi ya Anwar Ibrahim ni pigo la demokrasia:IPU

Umoja wa mabunge duniani, IPU umeeleza kukatishwa tamaa kwake na hukumu ya kifungo cha jela miaka mitano jela iliyotolewa na mahakama ya shirikisho nchini Malaysia dhidi ya kiongozi wa upinzani Anwar Ibrahim.

Ann Clwyd ambaye ni Rais wa kamati ya haki za binadamu za wabunge ndani ya IPU amesema hii ni mara ya pili kwa kiongozi huyo wa upinzani kuhukumiwa adhabu hiyo kwa makosa ya ulawiti kwenye nchi ambayo makosa kama hayo siyo ya kawaida.

Amesema taratibu za uendeshaji kesi hazikufuatwa hadi kutolewa kwa hukumu hiyo na kwamba IPU inaamini kuwa mashtaka dhidi yake yalikuwa na ushawishi wa kisiasa.

Kuridhiwa kwa hukumu hiyo ina maana kuwa Anwar ambaye sasa ana umri wa miaka 67 hatoweza kuwania kiti cha ubunge hadi miaka Sita baada ya kumaliza kifungo chake jela.