Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la Vienna lapitisha azimio kuhusu usalama wa nyuklia

Kongamano la Vienna lapitisha azimio kuhusu usalama wa nyuklia

Nchi wanachama wa Mkataba kuhusu Usalama wa Nyuklia, zimepitisha leo kwa kauli moja Azimio la Vienna kuhusu Usalama wa Nyuklia.

Azimio hilo ambalo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea kimataifa kuimarisha usalama wa nyuklia kufuatia ajali ya Fukushima-Daiichi, Japan, limepitishwa wakati wa kongamano la kidiplomasia ambalo limehitimishwa kwenye makao makuu ya Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, mjini Vienna.

Kongamano hilo liliandaliwa ili kutathmini pendekezo lililowasilishwa na Uswisi kufanyia marekebisho Aya ya 18 ya Mkataba kuhusu Usalama wa Nyuklia, ambayo inahusika na kubuni na kujenga mitambo ya nyuklia.

Rais wa kongamano hilo, ambaye pia ni mwakilishi wa Argentina kwa mashirika ya kimataifa mjini Vienna, Rafael Mariano Grossi, amesema kuwa kupitishwa azimio hilo ni habari njema kwa usalama wa nyuklia.