Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya makabiliano dhidi ya ugaidi yasisitiza utawala wa sheria

Kamati ya makabiliano dhidi ya ugaidi yasisitiza utawala wa sheria

Kamati ya makubaliano dhidi ya ugaidi ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa imekutana leo katika kikao maalum kilichoangazia umuhimu wa kuzingatia utawala wa sheria wakati wa mapambano dhidi ya vitisho vya ugaidi.

Akihutubia kamati hiyo waziri wa sheria wa Ufaransa Christiane Taubira amesema lazima kupambana na ugadi kote duniani, akisisitiza kuwa miongoni mwa vichocheo vya vitendo vya ugaidi ni umasikini na kwamba ukosefu wa huduma muhimu za kijamii kama vile elimu na afya huchochea makundi katika jamii kuwa na misimamo mikali kwa kuwa hawana cha kupoteza.

Hata hivyo amesisitiza..

(Sauti ya Taubira)

"Tunapaswa kujenga amani kupitia sheria, tunapswa kujua kwamba haitoshi kupigana na ugaidi ili kujenga amani endelevu. Tunapaswa kujenga amani bila kuweka kando utawala wa sheria, maadili yetu na uhuru wetu ambao unachukiliwa na magaidi, hasa uhuru wa wanawake"