Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau wakaribisha kuidhinishwa kwa baraza la mawaziri Somalia

Wadau wakaribisha kuidhinishwa kwa baraza la mawaziri Somalia

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, na wadau wake, wakiwemo Muungano wa Afrika, AU, mamlaka ya pamoja ya serikali kuhusu maendeleo, IGAD, pamoja na Muungano wa Ulaya, EU, wametoa taarifa leo, wakikaribisha kuidhinishwa kwa baraza jipya la mawaziri nchini humo, kulikofanywa na bunge mapema leo.

Wametoa wito kwa serikali, Waziri Mkuu na Bunge kuu kuenda mbele haraka kwa hatua itakayofuata, kupitia baraza hilo jipya la mawaziri.

Wameongeza kuwa wametiwa moyo na kujumuishwa kwa mawaziri wanawake kwenye baraza hilo.