Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mbinu endelevu ya wadau mbalimbali unahitajika ili kukuza utali wa kitamaduni

Mbinu endelevu ya wadau mbalimbali unahitajika ili kukuza utali wa kitamaduni

Mkutano wa utalii wa kitamaduni uliowaleta zaidi ya washiriki 900, ikiwa ni pamoja na zaidi ya mawaziri na makamu wa mawaziri 45 wa Utalii na Utamaduni, wataalamu wa kimataifa, wasemaji kutoka nchi 100, uliondaliwa na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na lile la utalii duniani, UNWTO uliofanyika Siem Reap nchini Cambodia umekamilika.

Lengo la mkutano huo ulikuwa ni kuchunguza na kuendeleza ushirikiano mpya kati ya utalii na utamaduni.

Katika taarifa UNESCO na UNWTO wamesema kila mwaka watalii zaidi ya bilioni moja huvuka mipaka ya kimataifa, wakiongeza kuwa hali hii inatoa uwezekano mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi duniani.

Utalii wa kitamaduni huongeza ushindani, hujenga fursa za ajira, kukabiliana na uhamiaji vijijini, kuzalisha kipato kwa ajili ya uwekezaji katika kuhifadhi, pamoja na  kuleta hisia ya kujivuna na kujithamini miongoni mwa jamii ya wenyeji.

Hata hivyo mashirika hayo yamesema kufanikisha, kukuza na kulinda urithi wa utalii wa kitamaduni kutategemea mbinu endelevu kutoka kwa wadau mbalimbali.