Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu 300 wasalia korokoroni DRC: OHCHR

Zaidi ya watu 300 wasalia korokoroni DRC: OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inaendelea na harakati za kuhakikisha watu walioshikiliwa kinyume cha sheria huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuatia maandamano ya kupinga sheria ya uchaguzi wanaachiliwa huru.Msemaji wa ofisi hiyo Ravina Shamdasani amesema watu zaidi ya 300 walikamatwa wakati wa maandamano hayo huko Kinshasa na Lubumbashi na 11 kati yao wanashikiliwa kwenye maeneo ambayo hakuna mawasiliano akiwemo mwakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali Christopher Ngoyi Mutamba.

 (Sauti ya Ravina)

“Tunarejelea wito wetu kwa mamlaka kuwaachia huru wanaoshikiliwa kwa kutekeleza haki yao ya msingi ya uhuru wa kukusanyika kwa amani na kutoa maoni yao, au kwa kujiunga na upinzani au kwa kupinga marekebisho ya sheria ya uchaguzi.”