Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mdungusi Kakati na manufaa yake kwa afya ya binadamu:FAO

Mdungusi Kakati na manufaa yake kwa afya ya binadamu:FAO

Mmea uitwao Dungusu kakati, au kwa kiingereza Cactus pear umetajwa na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kuwa zao la asili kwa mwezi huu wa Februari likiwa na manufaa kwa lishe na afya ya binadamu.

FAO inasema mmea huo wa jamii ya Mpungate hujulikana kama mkate wa maskini kwenye maeneo ya ukame kwani majani yake hupikwa mboga, maua, mbegu na matunda hutengenezwa siki au kuliwa yakiiva ilhali matawi yake ni lishe pia kwa mifugo.

Kiafya, matunda ya Dungusi Kakati yana kiwango kikubwa cha Vitamini C ilihali majani yake yanahusishwa na kupunguza kiwango cha sukari na lehemu kwenye mwili wa binadamu.

FAO pamoja na kuelezea mapishi ya mmea huo wenye miiba, imesema unaweza kuoteshwa kwa kutumia mbegu yake au tawi na asili yake ni Mexico lakini sasa umeenea hadi Kenya, Angola, Afrika Kusini na hata Marekani.