Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani mauaji ya mlinda amani Lebanon

Baraza la Usalama lalaani mauaji ya mlinda amani Lebanon

Wanachama wa Baraza la Usalama wamelaani vikali mauaji ya mlinda amani kutoka Uhispania ambaye aliuawa wakati wa mapigano yaliyoibuka tarehe 28, Januari, baina ya Israel na waasi walioko nchini Lebanon, katika maeneo ya mpakani.

Wanachama wa Baraza la Usalama wamepeleka salamu zao za rambirambi kwa familia ya mlinda amani huyo na serikali ya Uhispania.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano hii, wanachama hao wameelezea kutarajia haraka matokeo ya uchunguzi unaofanyika na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, ili kufahamu sababu ya kifo hicho.