Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2015 unanipa furaha na hofu kuhusu Somalia- Kay

Mwaka 2015 unanipa furaha na hofu kuhusu Somalia- Kay

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay, ameliambia Baraza la Usalama leo kuwa mwaka huu wa 2015 unampa hisia za furaha lakini pia hofu kuhusu hatma ya Somalia, akiongeza kuwa kuna kazi nyingi zaidi ya kufanya kuhusu taifa hilo mwaka huu kuliko mwaka uliopita. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Bwana Kay amesema ana furaha kwa sababu mwaka huu utakuwa wa maamuzi kuhusu hatma ya Somalia kama taifa lenye umoja na amani, huku akiwa na hofu kuhusu changamoto na hatari zilizopo. Akizungumza kuhusu umuhimu wa mchakato wa kisiasa mwaka huu Bwana Kay amesema hali itazidi kuwa tete uchaguzi wa mwaka ujao unapokaribia..

(Sauti ya KAY 1 )

Amemulika pia masuala ya kibinadamu, maendeleo na haki za binadamu, akisema ni lazima haki za binadamu zijumuishwe katika ujenzi wa taasisi zote. Akizungumza kuhusu hali ya usalama na amani, amesema kuwa imeimarika kwa kiwango kikubwa, lakini akaonya..

(Sauti ya KAY 2 )