Uchunguzi Gaza: Bi. Davis amrithi Profesa Schabas

3 Februari 2015

Kufuatia tangazo la kujiuzulu kwa Profesa William Schabas kama Mwenyekiti wa kamisheni ya Uchunguzi wa vita vya Gaza ya 2014, Rais wa Baraza la Haki za Binadamu, Balozi Joachim Ruecker amemteua Mary McGowan Davis kuchukua nafasi hiyoo.

Bi. Davis ni mwanachama wa sasa wa kamisheni hiyo na kwa mantiki hiyo, tume hiyo inasalia na wajumeb wawili, Bi. Davis akiwa mwenyekiti na Doudou Diène, ambao wote pamoja waliteuliwa mwezi  Agosti mwaka jana.

Taarifa ya Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa imesema tume hiyo inaendelea na kazi yake muhimu na imepangwa kuwasilisha utafiti wake kwa Baraza la Haki za Binadamu tarehe 23 mwezi Machi kama ilivyopangwa.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter