Kamati kuhusu kutoweshwa kwa watu yaanza kikao cha 8

2 Februari 2015

Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kutoweshwa kwa watu kwa lazima imeanza kikao chake cha nane leo Februari mjini Geneva.

Kikao hicho ambacho kitaendelea hadi tarehe 13 Februari, kinatazamia kutathmini ripoti za nchi tatu na kujadili suala la sheria ya kijeshi katika muktadha wa kulazimisha watu kutoweka. Akizungumza wakati wa kufunguliwa kikao hicho, mwenyekiti wa kamati hiyo Emmanuel Decaux, amesema kuwa ingawa kuna ripoti nyingi zinazowasilishwa, baadhi ya nchi wanachama, zikiwemo zile zilizoridhia mkataba husika, hazijafanya hivyo.

Amesema mkataba huo ni paa muhimu ambalo Kamati hiyo inapaswa kutumia kwa njia mwafaka.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter