Mfalme wa Uarabu akumbukwa na Baraza la Kuu

2 Februari 2015

Baraza kuu al Umoja wa Mataifa hii leo limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya kifo cha mfalme Abdullah Bin Abdulazizi Al-Saud wa falme za Uarabu aliyefariki dunia takribani wiki moja iliyopita. Taarifa zaidi an Joseph Msami..

(TAARIFA YA MSAMI)

(Nuts)

Mwendeshaji wa tukio hili anayemwakilisha Raisi wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa akitangaza ukimywa wa dakika moja kumbukumbuka kiongozi huyo anayeelezwa ni shujaa wa amani na maendeleo.

Wa kwanza kutoa salamu zake za heshima na kumbukumbu alikuwa Katibu Mkuu Ban ki-Moon ambaye amesema Mfamle Abdullah alikuwa kichocheo kikubwa cha amani katika ukanda wa nchi za Uarabuni na majadiliano ya tofauti za kiimani duniani.

Kwa upande wake mwakilishi wa kudumu wa Morocco katika Umoja wa Mataifa Omar Hilale amabye ameongea kwa niaba ya bara la Afrika amesema Mfalme Abdullah alifanya mengi lakini kubwa zaidi

(SAUTI OMAR)

Mwaka 2014 alitangaza mchango wa Saudi Arabia wa dola milioni 100 kwa ajili ya kuanzisha kituo cha Umoja wa Mataifa cha kupambana ugaidi. Mataifa ya Afrika yanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya mapambano dhidi ya ugaidi na vikundi vya ugaidi kama Boko Haram.

Baraza kuu pia limemkumbuka aliyekuwa mwakilishi wa Sweden katika Umoja wa Mataifa  Marten Grunditz ambapo viongozi kutoka kanda mbalimbali ikiwamo Asia na Ulaya wamewazelezea viongoz hao kuwa ni shupavu.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter