Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuwezeshe vijana walete mabadiliko:Ban

Tuwezeshe vijana walete mabadiliko:Ban

Baraza la uchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC leo limekuwa na jukwaa la vijana likiangazia kipindi cha mpito kutoka malengo ya milenia hadi malengo ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015 ukilenga kubaini mustakhbali wa vijana. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Jukwaa hilo lilijumuisha vijana wanaosaka ajira na hata wale walioko shuleni na vyuoni ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon katika hotuba yake akawaeleza bayana kuwa hali ya ajira duniani si shwari na kwamba fursa ya vijana kuajiriwa ni pungufu mara tatu zaidi ikilinganishwa na watu wazima. Hata hivyo akatanabaisha..

(Sauti ya Ban)

“Lakini vijana ni zaidi ya wahanga wa umaskini na mdororo wa kiuchumi. Vijana wanaweza kuwa waleta mabadiliko. Ndio maana ni lazime tuweke fursa za ajira kwa vijana na tusaidie wajasiriamali vijana ili waweze kuanzisha fursa za ajira kwa wenzao.”

Naye Rais wa ECOSOC Martin Sadjik akaweka bayana kuwa..

(Sauti ya Martin)

“Mmesikia kila mara, lakini ukweli ni kwamba nyie ndio mustakhbali! Na ninyi ndio mtakaohakikisha kuwa malengo ya maendeleo endelevu yanatimizwa.”