Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna wa UNRWA atembelea kambi ya wakimbizi Lebanon

Kamishna wa UNRWA atembelea kambi ya wakimbizi Lebanon

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina Pierre Krähenbühl ametembelea Lebanon na kukutabn na viongozi kadhaa wanchi hiyo akiwamo waziri mkuu wan chi hiyo Tamam Salam,na spika wa bunge Nabih Berri.

Taarifa ya UNRWA inasema katika ziara yake hiyo kamishina Krähenbühl ametembelea kambi ya wakimbizi iitwayo Nahr el-Bared na kukagua hatua za mradi wa ujenzi mpya .

Kamishina huyo pia amekutana na raia waliopoteza makazi walioko katika makazi ya muda pamoja na kukutana na kamati mashuhuri na makundi mengine kaskazini mwa Lebanon

Akizungumza wakati wa ziara hiyo amesema ilikuwa ni muhimu kwake kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nahr el-Bared na kuonyesha mshikamano wake kwa wakimbizi ambao wamefedheheshwa wakisubiri nyumba zao zijengwe.