IOM yalaani kubaguliwa kwa wahamiaji Afrika Kusini

30 Januari 2015

Shirika la Kimataifa la uhamiaji, IOM limelaani vurugu dhidi ya wahamiaji na wafanyi biashara wa kigeni katika mji wa Soweto ambayo sasa imeenea katika miji mengine kama vile Alexandra na Langlaagte. Taarifa Kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Kwa mujibu wa IOM vurugu hizo ni ukumbusho daima wa mazingira magumu ya wahamiaji nchini Afrika Kusini.

Mkuu wa Ujumbe wa IOM nchini Afrika Kusini, Richard Ots amesema kubaguliwa kwa wahamiaji kunachochea hisia za uporaji na uharibifu wa maduka ya wajasiriamali.

Joel Milman ni Msemaji wa IOM katika ofisi ya Geneva..

“Kuna hisia ambayo si sawa ya kwamba wahamiaji wanawasili Afrika Kusini ili kuchukua nafasi za kazi za wenyeji pamoja na kufaidika kutokana na mfumu wa kijamii, wakati hali halisi ni kwamba, wahamiaji wengi wanatengeneza nafasi za ajira na kuchangia kukua kwa uchumi ambao huwafaidisha raia wote wa Afrika Kusini”

Halikadhalika, IOM imeitaka serikali kufanya mazungumzo na wahamiaji na asasi za kiraia ili kujadili jukumu, msimamo na taswira ya wahamiaji nchini Afrika Kusini.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter